Tazama taarifa za mara kwa mara kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) katika nchi zote duniani.

COVID-19 ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Corona. Virusi hivyo vipya, Vilianzia nchini China mwezi Disemba mwaka 2019.

Imeelezwa kuwa dalili kuu za Corona ni pamoja na Homa kali, Uchovu na Kikohozi kikavu na nyingine zinatokea taratibu.

Dalili kubwa na inayoweza kutia hofu, ni mtu kukosa pumzi. Imeripotiwa, ni mtu 1 pekee kati ya watu 6 walioambukizwa virusi vya Corona hufikia dalili hiyo ya hatari. Na asilimia 80 ya walio na virusi hivyo hupata nafuu bila kuhitaji msaada wa matibabu.

Tazama hapa kujua hali ya Corona wakati wote duniani

Mkurugenzi aliyeshtakiwa uhujumu uchumi afariki
Video: Zitto amshauri Magufuli mambo 8 vita ya Corona

Comments

comments