Fuatilia hapa matangazo ya moja kwa moja kutoka Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museven akifanya mazungumzo ya faragha na Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.

Leo Agosti 9, 2018 Rais Yoweri Museven ametua nchini Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt. John Magufuli .

Atakuwa nchini kwa ziara ya siku moja ambapo lengo kubwa la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano na ujirani mwema uliopo kati ya Tanzania na Uganda.

Aidha, mazungumzo hayo yatafuatiwa na Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Mheshimiwa Rais Magufuli kwa heshima ya Rais Museveni na baadaye leo ataondoka nchini na wajumbe wake kurejea Uganda.

Tanzania yaandika historia Mkutano wa Kimataifa wa Manunuzi
Jack Grealish kubaki Aston Villa