Naibu Jaji Mkuu nchini Kenya, Philomena Mwilu amesema kuwa kushindwa kwa Tume ya Uchaguzi nchini humo (IEBC) kufuata agizo la mahakama kuhusu madai yaliyoibuliwa na upinzani, inaonyesha kuwa madai ya udukuzi yalikuwa ni ya ukweli.

Jaji Mwilu amesema mahakama ilikubaliana na madai ya upinzani kuwa matokeo yalitangazwa kabla ya matokeo yote kutoka kwa vituo 40,000 kupokelewa.

“Uchaguzi haukuwa na uwazi na hatukuwa na lingine ila kuufuta,” jaji amesema.

Tazama hapa moja kwa moja kutoka Kenya muda huu

Jaji huyo amesema tume ya IEBC ilitegemea ripoti za waangalizi wa uchaguzi kuamua kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki.

Waangalizi walikosolewa vikali wakati uchaguzi ulifutwa kwa kuharakisha kusema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wenye uwazi.

Aidha, Jaji Mkuu nchini Kenya, David Maraga amesema kuwa upinzani hakubaini madai yao kuwa kampeni za Rais zilitumia fedha za umma kugharamia kampeni zao.

Amesema kuwa sampuli kadha za fomu zilionyesha kuwa hazikuwa na mihuri rasmi, zingine hazikwa na sahihi na namba za usajili wala alama rasmi.

Amesema uchaguzi haukufutwa tu kwa sababu ulikuwa na hitilafu, lakini kile amekuwa akikichunguza ni ikiwa hitalafu hizo zilishawishi matokeo.

Picha za Young Dee na Amber Lulu zamkosanisha na mama yake
Mbowe anena mazito kuhusu Lissu