Tazama taarifa za mara kwa mara kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) katika nchi zote duniani.

COVID-19 ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Corona. Virusi hivyo vipya, Vilianzia nchini China mwezi Disemba mwaka 2019.

Imeelezwa kuwa dalili kuu za Corona ni pamoja na Homa kali, Uchovu na Kikohozi kikavu na nyingine zinatokea taratibu.

Dalili kubwa na inayoweza kutia hofu, ni mtu kukosa pumzi. Imeripotiwa, ni mtu 1 pekee kati ya watu 6 walioambukizwa virusi vya Corona hufikia dalili hiyo ya hatari. Na asilimia 80 ya walio na virusi hivyo hupata nafuu bila kuhitaji msaada wa matibabu.

Tazama hapa kujua hali ya Corona wakati wote duniani

Corona: Mabula ataka malipo ya kodi ya pango yalipwe kwa simu
Wagonjwa wa Corona waongezeka Tanzania wafikia 20

Comments

comments