Gwiji wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard, huenda akafanya mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya kurejea Merseyside.

Gerrard, anatarajiwa kufanya mazungumzo ya kurejea nyumbani, kufuatia uongozi wa klabu ya LA Galaxy inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Marekani (MLS), kumuarifu kuhusu suala la kutosaini nae mkataba mpya.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36, anatarajia kujikita kufundisha soka katika kituo cha kulea na kukuza vipaji kwa vijana cha Liverpool.

Mazungumzo ya kuomba ajira anatarajia kuyafanya na mkurugenzi wa kituo cha vijana cha Liverpool Alex Inglethorpe.

Wakati taarifa hizo zikichukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari, Gerrard pia anahusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu ya Celtic ya nchini Scotland pamoja na Newcastle Utd ya England.

MK Dons Kuivurugia Chelsea?
Mohamed Hussein Kubaki Msimbazi Kwa Miaka Miwili