Majogoo wa jiji Liverpool watapambana mwishoni mwa juma hili katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England dhidi ya Crystal Palace, bila ya beki pembeni Joe Gomez na kiungo Emre Can.

Meneja wa majogoo hao wenye maskani yao makuu Anfield mjini Liverpool Juergen Klopp, amethibitisha atawakosa wachezaji hao wawili katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema hii leo.

Gomez aliumia kifundo cha mguu wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya England na Uholanzi, uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita na The Three Lion waliibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 20 kutoka Engalnd, pia atakosa mchezo wa hatua ya robo fainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Manchester City utakaochezwa katikati ya juma lijalo.

“Ameumia sana, na sina budi kufuata ushauri wa daktari ili kumpa nafasi Gomez kupona kwa wakati, huenda ikamchukua hadi mwishoni mwa msimu huu kupona kabisa,” amesema Klopp

“Ni mtihani mkubwa kucheza bila ya Gomez, kwa sababu alikua ameshaanza kuzoea kupambana na kuiwezesha timu kuwa na uwiyano mzuri katika idara ya ulinzi.”

Kwa upande wa Emre Can anakabiliwa na majeraha ya mgogo alioyapata wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Hispania, hali ambayo ilimfanya aukose mchezo dhidi ya Brazil uliomalizika kwa Ujerumani kufungwa bao moja kwa sifuri.

John Stones kuikosa Everton
Nape: Bila kuvumiliana kisiasa Tanzania itakuwa nchi ya hovyo