Majogoo wa jiji Liverpool wataumana na Manchester City katika hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa mujibu wa droo iliofanyika leo mchana.

Liverpool na Man City ndio timu pekee kutoka England zilizotinga hatua hiyo baada ya Tottenham Hotspur, Manchester United na Chelsea kutolewa hatua ya 16 bora.

Liverpool itaanzia Anfield kabla ya kwenda Etihad Stadium kuwafuata wapinzani wao.

Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Real Madrid wamepangwa kucheza na Juventus wakati Barcelona wakipewa AS Roma.

Sevilla amepangiwa kucheza na mabingwa wa Ujerumani timu ya Bayern Munich.

Ratiba kamili ya robo fainali ya klabu bingwa

Barcelona vs AS Roma

Sevilla VS Bayern Munich

Juventus vs Real Madrid

Liverpool VS Manchester City

UEFA Europa League: Arsenal wapelekwa Urusi
Mashabiki wa Mbao FC wautaka uongozi kujitathmini