Majogoo wa jiji Liverpool wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Misri na klabu ya AS Roma ya Italia Mohamed Salah, kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 40.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, amekua katika mawindo ya meneja wa Liverpool Jurgen Klopp, ambaye anaamini uwezo wake tangu alipokua Chelsea.

Taarifa zilizothibitishwa na shirika la utangazaji la Uingereza BBC, zinaeleza kuwa, mazungumzo ya uhamisho wa mshambuliaji huyo yanaendelea vizuri, na huenda wakati wowote kabla ya mwishoni mwa juma hili Salah atafanyiwa vipimo vya afya.

Endapo Liverpool watakubali kutoa Pauni milioni 40 kama ada ya uhamisho wa mshambuliaji huyo, watakuwa amevuka kiwango cha usajili ambacho hawakuwahi kukitumia tangu walipomsajili Sadio Mane kwa Pauni milioni 34.

74 Wachukua Fomu, Kurejesha TFF
Video: LHRC walaani shambulio la walemavu, wataka Jeshi la Polisi DSM liombe radhi