Timu ya Liverpool imeanza mazungumzo na winga wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain, 23, ambaye huenda akagharimu pauni milioni 25, huku Manchester City na Chelsea zikimnyatia.

Aidha, Liverpool wanataka kumsajili winga huyo wa Arsenal ili kuweza kujiimarisha na kuijweka sawa katika msimu ujao ambao wamedhamilia kutwaa ubingwa.

Liverpool imedhamilia kuleta upinzani mkubwa katika ligi kuu ya Uingereza msimu ujao ili kuweza kuweka uwezekano wa kutwaa kombe la ligi ya nchi hiyo EPL.

Hata hivyo, tofauti na Liverpool timu za Manchester City na Chelsea zinamnyatia mchezaji huyo mwenye kasi ya ajabu ambaye ameonekana kusugua benchi katika timu yake ya Arsenal.

 

Je kiswahili kitumike kama lugha ya kufundishia ngazi zote za elimu?
Gambo awapiga dongo wapinzani, asema kama hawatabadilika watapotea