Majogoo wa jiji Liverpool wamepanga kumtumia mshambuliaji wao kutoka nchini Italia Mario Balotelli kama chambo, katika vita ya kumuwania kiungo wa klabu ya SS Lazio, Lucas Biglia.

Balotelli ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya AC Milan kwa mkopo, ameshindwa kujihakikishia nafasi ya kusalia mjini Milan kutokana na kuonyesha kiwango kibovu na mwishoni mwa msimu huu anatarajia kurejea Anfield katika klabu yake ya Liverpool.

Kutokana na jambo hilo viongozi wa The Reds, wanaona kuna umuhimu wa kumpa nafasi nyingine Balotelli kucheza soka akiwa nchini kwao Italia kwa kumuingiza kwenye mipango ya kumpeleka SS Lazio sambamba na kiasi kidogo cha pesa ili kumpata Biglia.

Liverpool wamejipanga kufanya hivyo kutokana na upinzani mkubwa ambao huenda wakakutana nao katika harakati za usajili wa kiungo huyo kutoka nchini Argentina ambaye pia yupo kwenye rada za klabu za Real Madrid na FC Bayern Munich.

Lucas Rodrigo Biglia

Taarifa zilizotangazwa na kituo cha televisheni cha Sky Italia, zineeleza kwamba Liverpool wana matarajio makubwa ya kunasa Biglia mwenye umri wa miaka 30 kwa kutumia mbinu za kumjumuisha Balotelli katika dili hilo.

Inaaminika kuondoka kwa mshambuliaji kutoka nchini Ujerumani Miroslav Klose kwenye klabu ya SS Lazio itakapofika mwishoni mwa msimui huu, itakua ni rahisi kwa viongozi wa klabu hiyo ya mjini Roma kumkubali Balotelli.

Juventus Watetea Ubingwa Wa Scudetto Kwa Mbwembwe
Video Mpya: Colors of Africa - Mafikizolo Feat. Diamond & Maphorisa