Mahasimu wa soka nchini England Liverpool na Manchester United watacheza mchezo wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi nchini Marekani, katika michuano ya kombe la mabingwa wa kimataifa (International Champions Cup) mwezi Julai mwaka huu.

Mahasimu hao watacheza mpambano huo katika uwanja wa Michigan (The Big House) wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 107,000 walioketi.

Uwanja huo ulitumika mwaka 2014 katika mchezo wa kujiandaa na msimu wa 2014/15 kati ya Man Utd dhidi ya Real Madrid na kuhudhuruwa na mashabiki 109,000 walioketi.

Uwanja wa huo ni uwanja wa pili kwa ukubwa duniani ukitanguliwa na uwanja wa 1 May uliopo mjini Pyongyang, Korea kaskazini wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 114,000.

Kwa mara ya mwisho Liverpool na Man Utd walicheza mchezo wa kujiandaa na msimu mwaka 2014/15 mjini Miami nchini Marekani, na kikosi cha mashetani wekundu kilichokua kikiongozwa na Louis van Gaal kwa wakati huo kiliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja.

Michuano ya ICC ambayo inaendelea kuwa na umaarufu duniani kwa mwaka 2018 itashirikisha klabu kubwa kama Real Madrid, AC Milan na Juventus.

Uingereza yashindwa kupeleka waamuzi kombe la dunia 2018
Wilder agoma kuhudhuria pambano la Joshua na Parker kisa ‘ubabe’

Comments

comments