Huenda majogoo wa jiji Liverpool hawajafahamu ni nani anaepaswa kukabidhiwa jukumu la kupewa nafasi ya ushambuliaji kuanzia msimu ujao, kutokana na hatua zao za kumsaka mtu huyo kuonyesha hali ya kutoaminiana wao kwa wao.

Klabu hiyo ya Anfield, mapema hii leo imeripotiwa kuingia katika harakati za kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka Uruguay na klabu bingwa nchini Ufaransa PSG, Edinson Cavani.

Tayari wababe hao wa jiji la Liverpool wamehusishwa na mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Argentina na klabu ya SSC Napoli Gonzalo Higuain kutokana na harakati zao za kuwa mbioni kumuweka sokoni Christian Benteke ambaye ameonekana haendani na mfumo wa Jurgen Klopp.

Hatua ya kugeukia kwa Cavani, ineonyesha bado kuna tatizo la mkakati wa usajili wa mchezaji anaecheza nafasi ya ushambuliaji ndani ya klabu hiyo.

Cavani, mwenye umri wa miaka 29 amekua katika hali ya kutoifahamu hatma yake ndani ya PSG, licha ya kuondoka kwa mshambuliaji kutoka nchini Sweden, Zlatan Ibrahimovic kwa kile kinachotajwa kutokua na maelewano na meneja wa klabu hiyo Laurent Blanc.

Kenya yapiga Marufuku maandamano
Sascha Fligge: Hatujui Lolote Kuhusu Mazungumzo Ya Aubameyang