Majogoo wa jiji Liverpool ni miongoni mwa timu ambazo zinasubiri droo ya hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa League, baada ya kufanikisha azma ya kupata matokeo mazuri katika mpambano wa hatua ya 16 bora dhidi ya mashetani wekundu, Man Utd usiku wa kuamkia hii leo.

Liverpool walilazimisha matokeo ya sare ya bao moja kwa moja katika mchezo huo, ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Old Trafford, hatua ambayo iliwawezesha kuondoka na ushindi wa jumla mabao matatu kwa moja, kufutia ushindi waliouvuna kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa juma lililopita.

Katika mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo, Man Utd walikua wa kwanza kupata bao kwa njia ya mkwaju wa penati, iliyopigwa na mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Anthony Martial dakika ya 32 kipindi cha kwanza, lakini dakika 13 baadae Philippe Coutinho aliisawazishia Liverpool.

Timu nyingine zinazosubiri droo ya hatua ya robo fainali katika michuano ya Europa League ni Borussia Dortmund, Sevilla, Shakhtar Donetsk, Villarreal, Sparta Prague, Athletic Bilbao pamoja na Sporting Braga.

Matokeo ya jumla katika michezo ya hatua ya 16 bora kwenye michuano hiyo ya Europa League.

Valencia 2 – 1 Ath Bilbao (Agg 2-2)

Athletic Bilbao wameshinda kwa faida ya bao la ugenini

Man Utd 1 – 1 Liverpool (Agg 1-3)

Tottenham 1- 2 Bor Dortmd (Agg 1-5)

Bayer Levkn 0 – 0 Villarreal (Agg 0-2)

Lazio 0 – 3 Sparta Prague (Agg 1-4)

Anderlecht 0 – 1 Shakt Donsk (Agg 1-4)

Sevilla 3 -0 FC Basel (Agg 3-0)

Sporting Braga 4 – 1 Fenerbahçe (Agg 4-2)

Muhimu: kwenye mabano ni jumla ya mabao yaliyofungwa katika michezo ya nyumbani na ugenini.

Mshauri mkuu wa Maalim Seif anasa mikononi mwa polisi
Mustakabali Wa Yaya Toure Bado Upo Shakani Man City