Beki wa kati kutoka nchini Ubelgiji, Thomas Vermaelen huenda akarejea nchini England, kufuatia FC Barcelona kuonyesha nia ya kukubali kumuachia.

FC Barcelona wamefikia hatua hiyo, baada ya kutoridhishwa na huduma ya Vermaelen tangu alipojiunga nao mwaka 2014, akitokea Arsenal FC ya kaskazini mwa jijini London.

Tayari klabu za Liverpool na West Ham United zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili beki huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye hakupata nafasi ya kucheza ipasavyo akiwa na FC Barcelona kufuatia majeraha ya mara kwa mara.

Kwa mujibu wa mtandao wa Spanish publication Sport, Vermaelen ameonyesha kuwa tayari kurejea nchini England, kwa kuamini atakapofanikisha safari hiyo itakua ni rahisi kwake kucheza kila juma tofauti ilivyo sasa huko Camp Nou yalipo makao makuu ya FC Barcelona.

West Ham United wameshaweka wazi mpango wao wa kusaka beki wa kati katika kipindi hiki cha kuelekea msimu mpya wa ligi, kutokana na mapungufu yaliyojitokeza msimu uliopita klabuni hapo.

Meneja wa The Hammers, Slaven Bilic anaamini Vermaelen anakidhi haja ya kuwa sehemu ya kikosi chake kutokana na uzoefu alionao wa kucheza katika ligi ya nchini England.

Kwa upande wa Liverpool nao wanahitaji kufanya usajiali wa beki wa kati, kutokana na changamoto inayowakabili kwa sasa ya kuwaachia Martin Skrtel na Kolo Toure.

Meneja wa majogoo hao wa jiji, Jurgen Klopp ana nia kama ilivyo kwa Bilic ya kuona Vermaelen anafaa kwa kigezo cha kuwa na uezofu wa kutosha wa kucheza ligi ya nchini England.

Chelsea Kuokota Dodo Chini Ya Mpera?
Southampton Wamgeukia Frank De Boer