Michezo ya kuwania kufuzu kwenye mashindano ya Vilabu bingwa barani Ulaya yameanza hapo jana ambapo michezo kadhaa ilichezwa huku Klabu ya Liverpool kutoka Uingereza ikiibuka na ushindi wa magori 2-1 ugenini dhidi ya Hoffinhem ya nchini Ujerumani

Liverpool waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao hayo mawili kwa sifuri huku mabao ya Liverpool yakiwekwa kimiani na Alexandre Arnold dakika ya 35 na James Milner dakika ya 74 huku la Hoffeinheim likifungwa na Mark Uth dakika ya 87.

Aidha, michezo mingine iliyopigwa hapo jana kuwania kufuzu michuano hiyo ni pamoja na ule wa Klabu ya Sporting Cp ya nchini Ureno na FC FCSB ambao  awalitoka suluhu ya bila kufungana na FC FCSB, huku  CSKA Moscow nao wakatoka sare ya bila kufungana na Young Boys.

 

Mke wa Mugabe awaponyoka polisi Afrika Kusini na tuhuma za kumpiga mrembo
Mabilioni ya Escrow yaliyotoroshwa sasa kurejeshwa nchini