Klabu ya Liverpool jana usiku ilifanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 3- 0 dhidi ya timu ya Manchester City katika mashindano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya, mchezo uliopigwa katika dimba la Anfield.

Liverpool imetinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kabisa kwa mara ya kwanza tangu ilivyofanya hivyo mwaka 2008, hali iliyofanya mashabiki kufurika kwa wingi na kushuhudia mpambano huo mkali uliochezwa katika dimba la Anfield.

Aidha, wachezaji waliofunga mabao ni Mohamed Salah ambaye alifunga bao katika dakika ya 12, Alex Oxlade-Chamberlain na Sadio Mane yote yakifungwa katika kipindi cha kwanza.

 

Majambazi wavunja kanisa la Mt. Theresia, Mbezi
Uturuki, Iran na Urusi zaungana kuisaka amani nchini Syria

Comments

comments