Michuano ya klabu bingwa hatua ya makundi imeendelea usiku wa jana ambapo michezo 8 imepigwa katika viwanja tofauti, Liverpool wakicheza ugenini katika uwanja wa Ljudski vrt wameichapa Maribor mabao 7-0.

Mabao ya Liverpool yalifungwa na Robert Firminho aliyefunga 2, Mohamed Salaah akifunga mabao mawili pia, huku Alex Oxlaide Chamberlain, Phillipe Coutinho na Alexander Anord pia wakicheka na nyavu.

Ushindi huo unaifanya  Liverpool kuwa timu ya nne kuwahi kufunga jumla ya mabao 7 na zaidi ambapo timu za Bayern Munich, Barcelona na Lyon zimewahi kufanya hivyo na kizuri zaidi Liverpool haikuruhusu bao.

Real Madrid  wakiwa Santiago Bernabeu wakiikabiri Tottenham  almanusra waambulie kichapo baada ya bao la kujifunga la Rafael Varane lakini dakika ya 43 ya mchezo Cristiano Ronaldo aliwaokoa Madrid kwa mkwaju wa penati.

Tottenham Hotspur wanakuwa timu ya tatu kuwahi kupata alama katika uwanja wa Santiago Bernabeu katika michezo ya Madrid 24 iliyopita katika Champions League baada ya suluhu ya 1-1 waliyoipata jana.

Manchester City waliipiga Napoli bao 2 huku Gabriel Jesus akifunga moja ya bao linalomfanya kufunga mabao 15 ndani ya michezo 22 ikiwa ni mchezo mmoja nyuma ya Kun Aguero wakati anafunga mabao kama hayo alipofika Man City.

Kwingineko bao la Papstathopoulos liliookoa Dortmund kutoka katika kipigo na kuwafanya kutoka sare ya moja kwa moja dhidi ya Apoel Nicosia, huku Monaco wakifungwa 2 kwa 1 na Bestikas katika uwanja wao wa nyumbani.

Sevilla walijikuta wakiaibika kwa bao 5 kwa 1 kutoka kwa Spartak Moscow huku mabao ya Moscow yakiwekwa kimiani na Luiz Adriano, Promez, Giushakov na Dzhkiya.

Daraja la Momba kuongeza kasi ya uzalishaji
Serikali yalipa Bilioni 190 kwa kipindi kifupi