Bao la Tiki- Taka la dakika ya 45 kipindi cha kwanza la kiungo kutoka Ujerumani Emre Can, limeipa Liverpool pointi tatu muhimu mbele ya Watford, katika mchezo wa ligi kuu England uliochezwa usiku wa kuamkia leo huko Vicarage Road.

Can amefunga bao hilo ambalo huenda likaingia kwenye kinyang’anyiro cha kusaka bao bora msimu huu, baada ya kuunganisha pasi safi ya Lucas Leiva, akiwa katikati ya mabeki wawili wa Watford na kuutia mpira wavuni.

Aisha, katika mchezo huo ilishuhudiwa Liverpool ikilazimika kufanya mabadiliko bila kupenda katika dakika 15 za kipindi cha kwanza baada ya kiungo wake Philippe Coutinho kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Adam Lallana.

Ushindi huo umeifanya Liverpool ibaki nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 66. Pointi tatu mbele ya Man City na pointi nne mbele ya Manchester United inayoshika nafasi ya tano.

Young Africans Washtukia Mbinu Chafu
Picha 10: Rais Magufuli katika kilele cha sikukuu ya wafanyakazi Duniani