Licha ya kutawala mchezo wa leo kwa asilimia kubwa klabu ya Liverpool ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani (Anfield) imelazimishwa sare ya 0-0 na Manchester United.

Kikosi hicho cha Jurgen Klopp kilitawala mchezo kwa muda mrefu na kilishambulia lango la United mara 19 lakini kipa David De Gea alikuwa imara na kuwazuia.

United ilionekana kuzembea katika safu ya ushambuliaji wakati mshambuliaji Romelu Lukaku akikosa bao dakika chache kabla ya kwenda mapunziko kwa kupiga shuti kali lililookolewa na mlinda mlango Simon Mignolet.

Kipindi cha pili Liverpool walizidi kutawala mchezo lakini Emre Can alipoteza nafasi ya wazi ya kufunga bao baada ya kupiga shuti lililopaa juu na mpaka dakika ya 90 matokeo yalikuwa 0-0.

Liverpool hawajapata ushindi dhidi ya Man Utd tangu mwaka 2014 walipoipiga Manchester United bao 3 kwa 0 na wanazidiwa pointi 7 na Man Utd ktika msimamo wa ligi kuu.

 

 

Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 15, 2017
Video: Sitafuta Mwenge kamwe katika uongozi wangu- JPM