Klabu ya Liverpool imefanikiwa kufuzu kuingia katika hatua ya makundi ya Ligi ya Klabu Bingwa Barani Ulaya (UEFA) mara baada ya kuichapa timu ya Hoffenheim ya Ujerumani magori 4-2 hivyo kuwa na jumla ya magori 6-3.

Ushindi huo dhidi ya Hoffenheim umeifanya Liverpool kuwa Klabu ya Tano kwa Uingereza kufuzu kucheza michuano hiyo, hivyo kwa mara ya kwanza England itawakilishwa na timu tano katika hatua ya makundi ya Ligi ya  Mabiingwa Barani Ulaya

Aidha, kwa upande wa Hoffenhem walioshindwa kufuzu katika michuano hiyo, katika Ligi yao nchini Ujerumani msimu uliopita walishika nafasi ya nne, hivyo walikuwa na matumaini makubwa ya kufuzu katika mashindano hayo makubwa barani humo.

Liverpool walikuwa wakiongoza 2-1 kutokana na mechi ya kwanza, hivyo katika mechi hiyo ya marudianao walihakikisha mambo hayawezi kuwageuka kwa kufunga mabao matatu dakika 20 za kwanza za mechi mechi hiyo ya marudiano.

Hata hivyo, Vilabu vya Liverpool, Chelsea, Tottenham, Manchester City na Manchester United vimeingia katika droo ya makundi ya ligi hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika hii leo ambapo kila mmoja atajua amepangwa kundi gani.

 

Hofu Yatanda Kambi Ya Ruvu Shooting
TFF Yaomba Radhi Kwa Kosa La Maandishi