Gwiji wa klabu ya Arsenal Freddie Ljungberg ameonyesha kuwa na matumaini makubwa na meneja Arsene Wenger, msimu huu kwa kusema huenda tatizo la kutwaa ubingwa wa Uingereza likafikia tamati kutokana na usajili mzuri alioufanya.

Ljungberg ambaye aliitumikia Arsenal kuanzia mwaka 1998 hadi 2007 amesema tatizo kubwa ambalo Wenger lilikua likimsumbua na kushindwa kufikia hatua ya kutwaa ubingwa wa ligi nchini Uingereza, ni mipango ya usajili wa wachezaji ambao waliwahi kuwanao misimu kadhaa iliyopita.

Amesema kwa sasa meneja huyo kutoka nchini Ufaransa amefanya usajili mzuri ambao unaanza kumuanisha hakuna kitakachoshindwa kumfikishia lengo la kuwafurahisha mashabiki wa Arsenal ulimwenguni kote.

Ljungberg anaamini uwepo wa wachezaji kama Granit Xhaka na Lucas Perez katika kikosi cha The Gunners kitaleta mapinduzi ya kiushindani baina ya wachezaji.

Image result for Granit Xhaka and Lucas PerezGranit Xhaka (kushoto) akishangilia baada ya kufunga bao lake la kwanza dhidi ya Hully City,  Lucas Perez (Kulia) akimpongeza

 “Uwezo wa mchezaji kama Xhaka ninaamini ni hatua nzuri kwa Arsenal ambayo kwa muda mrefu ilimuhitaji mtu kama huyu.

“Tangu amekuja Emirates na kila anapopewa nafasi, anaonyesha kujituma kwa kusaidiana na wengine na inapobidi anaonyesha uwezo binafsi na kuisaidia Arsenal kufikia lengo la ushindi,

“Ninaweza kumfananisha na kiungo ambaye aliwahi kutamba akiwa na Arsenal (Emmanuel Petit).

“Kwa upande wa Lucas ameninivutia kwa namna anavyocheza na ananiminisha katika nafasi ya ushambuliaji msimu huu kutakua na ushindani mkubwa sana.

“Wakati wa nyuma baadhi ya mashabiki walihitaji kuona Wenger anafanya usajili wa wachezaji ambao wangeisaidia Arsenal kufikia malengo, naamini kwa msimu huu jambo hilo limepata ufumbuzi na litaleta mafanikio makubwa.” Alisema gwiji huyo aliyecheza michezo 216 na kuifungia Arsenal mabao 72.

Ljungberg, kwa sasa ni kocha wa kituo cha kulea na kuendeleza vipaji vya watoto cha Arsenal.

Ryan Giggs Kumrithi Francesco Guidolin?
Lakuvunda Halina Ubani, Kompany Ashindwa Tena

Comments

comments