Lori la mafuta limewaka moto na kuteketea katika eneo laNgiloli wilayani Gairo Mkoani Morogoro

Akitoa taarifa za awali Mwandamizi wa Jeshi la polisi Wilbroad Mutafungwa amesema dereva wa lori hilo Rashid Hamza mkazi wa Mkolani Mwanza ameshikiliwa na polisi kwaajili ya uchunguzi.

Kwa mujibu wa maelezo ya dereva wa lori hilo amesema alipofika kwenye kilima aliamua kushuka na kupaki gari kwenda kununua mua wa kula wakati amemaliza kununua miwa alivyorudi kwenye gari akaona gari linaserereka uku likiwa linarudi nyuma na aakajitaidi kuingia kwenye gari ili kufunga break za gari ikashindikana.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Gairo Seriel Mchembe amewapongeza Tanesco kwa kukata umeme haraka maana kuna nyumba ilianza kuwaka moto. Sambamba na hilo Afisa wilaya ya Gairo alisaidia kuzima moto iliyoanza kwa fire extuingisher ndogo ndogo alizokuwanazo nyumbani kwake.

“Hapa uwa panauzwa sana mafuta ya vidumu lakini kwakweli neema za mungu zimonekana leo yaani kama kuna mungu basi leo gairo tuseme mungu ametusaidia” Amesema Mchembe.

JPM awasilisha fedha za ujenzi wa msikiti
Msolla: Sikumaanisha kama ilivyopokelewa