Meneja wa kilabu ya Manchester United, Louis Van Gaal amesema hana wasiwasi kuhusu kibarua chake huku akionyesha kuwa na matarajio makubwa na kikosi chake ambacho kimepoteza nafasi ya kuendelea kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

United iko katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ya England, ikiwa pointi tatu nyuma ya viongozi Leicester City, lakini imekosolewa kwa kushindwa kufunga mabao na kuonyesha mchezo mzuri msimu huu.

United lipoteza 3-2 kwa Wolfsburg siku ya jumanne, hali ambayo ilidhihirisha kuondoshwa kwao kwenye michuano ya barani Ulaya msimu huu na sasa watashiriki Europa League hatua inayofuata.

”Nafanya bidii, ili kufanya tunachoweza kufanya”, alisema meneja huyo mwenye umri wa miaka 64.

Na alipoulizwa iwapo alihisi wasiwasi wowote kuhusu kibarua chake alijibu, sina wasiwasi, lazima ushinde na kushindwa katika michezo na hilo lazima likubalike.

”Tatizo ni kwamba lazima tukabiliane na matarajio, katika kilabu kama hii ni mengi mno” aliongeza Van Gaal.

Man Utd hii leo inashuka dimbani kupambana na AFC Bournemouth katika muendelezo wa michezo ya ligi ya nchini England.

Jose Mourinho Na Matarajio Ya Kuvuka Daraja Lililo Mbali
Platini Kuendelea Kusota Jela Ya Soka