Meneja wa Man Utd, Louis van Gaal usiku wa kuamkia hii leo, alishindwa kujizuia na kujikuta akimtusi mshambuliaji wake kutoka nchini Ufaransa Anthony Martial kwa kumuita mpambavu.

Van Gaal, alifikia hatua hiyo, baada ya kuchukizwa na matokeo ya mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo, Man Utd walikua ugenini huko nchini Urisi, wakipambana na CSKA Moscow, na kulazimika matokeo ya bao moja kwa moja.

Meneja huyo kutoka nchini Uholanzi, amesema Martial alionyesha kitendo cha kipuuzi kwa kukubali kuushika mpira katika eneo la hatari kwa makusudi na kuwazawadia wenyeji penati iliyowapa bao la kuongoza.

Hata hivyo alipoulizwa ni vipi alivyojihisi pale mshambuliaji huyo aliyemsajili akitokea AS Monaco, alipofunga bao la kusawazisha, Van Gaal alisema ni jambo la kawaida kutokea kwani ni wajibu wake kufunga lakini haikua wajibu wake kuushika mpira kwa makusudi eneo la hatari.

Martial, alifanya makossa kwa kuunawa mpira kwenye eneo la hatari la Man Utd katika dakika ya 15, kufuatia mpira uliokua umepigwa na Mario Fernandes wa CSKA Moscow.

Hata hivyo mkwaju wa penati uliopigwa na Roman Eremenko baada ya tukio hilo kutokea iliokolewa na mlinda mlango David de Gea, lakini mshambuliaji kutoka nchini Ivory Coast, Seydou Doumbia alifanikiwa kuuwahi mpira na kufunga bao upande wa CSKA Moscow.

Eden Hazard Atikisa Kibiriti Chelsea
Alichokisema Nape Baada Ya Kupata Ajali Mbaya Ya Gari