Matukio mengi yamejitokeza huku mengine yakiwa yameacha sintofahahamu katika vichwa vya wengi, huku msemo wa matukio ya kumbukumbu yakijirudia kuwa kumbukumbu siyo lazima iwe nzuri bali hata ile inayohuzunisha hubaki kuwa kumbukumbu. Yafuatayo ni baadhi ya matukio makubwa yaliyojitokeza mwishoni mwa wiki hii.

Lowassa Kuzungumza Yamoyoni.

Mjumbe wa kamati kuu Chadema na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa wakati akifanyiwa mahojiano na Azam two alieleza mambo mengi kutokana na maswali aliyokuwa akiulizwa na Mtangazaji Tido, ambapo katika suala la kusimamia elimu bora Mh Lowassa alisema ili kuwa na Elimu bora maslahi ya waalimu yanatakiwa kuboreshwa kwanza kabla ya kushughulikia madawati.

mkuu_lowasa2

Aidha katika maswali ambayo yalijibiwa na kiongozi huyoni pamoja na kuweka wazi kutozungumia suala la ricmond na kusema lilipofika inatosha na sasa watu wafanye mambo mengine siyo kuzungumzia jambo moja miaka 10 huku katika maelezo mengine akisema CCM ilimhukumu pasipo kumpa nafasi ya kujitetea.

Mahafali ya MUHAS Kusisitishwa.

Tarehe 30 ya mwezi wa saba uongozi wa chuo kikuu cha Afya na sayansi shirikishi MUHSA kilisitisha mahafali ambayo yalitakiwa kufanyika chuoni hapo na kutoa agizo la wanafunzi kutojishughulisha na mikusanyiko ya kisiasa.

MUHAS

Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa chuo Prof. Apolnary Kamuhabwa kupitia tangazo lililobandikwa chuoni hapo alinukuliwa kuwaonya wanafunzi kutoweka mijusanyiko na kutojishughulisha na masuala ya kisiasa kama ilivyo kwa watumishi wa umma.

Uzinduzi wa Klobaa App.

Usiku pia wa Jumamosi ulizunduliwa mtandao ”Klobaa app” utakao waunganisha watumiaji na matukio mbalimbali ya burudani na matukio ya usiku katika majiji mbalimbali huku kundi la Navy Kenzo wakiwa wamechaguliwa kuwa Mabalozi wa App hiyo.

klobaa

Perrycurtis Elechi Akizungumzia kuhusu Klobaa alidai kuwa waliamua kuwachukua Navy Kenzo kama mabalozi wao kutokana na hatua kubwa kimuziki waliyofikia. Klobaa app ni mtandao ulioanzishwa Marekani 2015 na sasa imesajiliwa kufanya biashara nchini.

Mbowe Kuitwa Polisi.

Kiongozi Mkuu wa upinzani na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe jana alifika kituo kikuu cha polisi dar es salamm kwa mahojiano ambapo alisindikizwa na wanasheria Tundu Lissu pamoja na Preter Kibatala huku baadhi ya viongozi waliomsindikiza wakizuiliwa.

mbowe..........

Mbowe aliitwa siku ya juzi na ofisa wa upelelezi kanda maalumu ya Dar es salaam kwa tuhuma za uchochezi na siku ya jana alihojiwa kwa saa 2 mbele ya wanasheria watatu wa  chama Tundu Lissu, John Mallya, na Fred Kalonga baadae kuachiwa kwa dhamana.

Wakili Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki naye anakabiliwa shtaka la uchochezi hivyo aliitaka Serikali kutoa maana ya neno ‘uchochezi’ ili wakati mwingine upinzani waweze kuliepuka kutumia.

 

Video: 'Serikali yangu haihitaji kodi za watu wanyonge' - Magufuli
Mohamed Dewji "Mo" Awashukuru Wanachama Wa Simba