Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa amedai kuwa mhubiri maarufu wa Nigeria, TB Joshua amemtabiria ushindi katika uchaguzi mkuu ujao (2020).

Akizungumza jana katika kikao cha ndani Mkoani Tabora, Lowassa alisema kuwa mhubiri huyo ambaye alikuja nchini siku chache baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu alikihakikishia chama hicho maono ya ushindi katika uchaguzi ujao.

“Najua waandishi wa habari wataandika, lakini sijali, rafiki yangu TB Joshua ametabiri Serikali ijayo itangozwa na Chadema,” Lowassa anakaririwa na Mwananchi.

Hata hivyo, Lowassa aliwaeleza viongozi hao kuwa mhubiri huyo alitoa masharti kuwa ili utabiri huo uweze kutimia ni lazima washikamane na wadumishe umoja ndani ya chama hicho.

Kabla ya kujiunga na Chadema, Lowassa ni mmoja kati ya wanasiasa walioenda nchini Nigeria na kuombea na TB Joshua. Rais John Magufuli pia pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba walifika katika kanisa la Synagogue Church of All Nations (SCOAN) na kuombea na mhubiri huyo kabla ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha urais.

Bosi mtandao wa jamii forums mbaroni
Lewandowski: Naamini Kwa Pamoja Tutafanikisha Malengo