Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anaeungwa mkono na vyama vya upinzani vinanavyounda Ukawa, Edward Lowassa ameendelea kukishukia Chama Cha Mapinduzi kwa madai kuwa kilishindwa kuleta maendeleo yaliyotakiwa kwa wananchi kulingana na muda kilichokaa madarakani.

Akiongea jana na katika mkutano wa kampeni katika jimbo la Vunjo, Lowassa aliwataka wananchi kuikataa CCM kwa kuwa kwa muda wa miaka 50 imekuwa ni miaka ya shida.

“Miaka 50 ya CCM ni shida,” alisema Lowassa kabla ya kuwasisitiza wananchi kumchagua yeye na wagombea ubunge na udiwani wa vyama vya upinzani vinaunda Ukawa kwa kuwa wamejipanga kuwaletea wananchi maendeleo kwa kasi aliyoiita ‘speed 120’.

Alisema CCM imeshindwa katika kipindi chote na sasa kitasombwa na mafuriko ya kura za wananchi ifikapo Oktoba 25 na kwamba huo ndio utakuwa mwisho wake.

Alisisitiza kuwa nia yake ni kuhakikisha anaondoa umasikini wa wananchi na kuongeza kipato chao mara dufu ili anaepata mlo mmoja aweze kula milo miwili. Hivyo, aliwataka wananchi hao kuhakikisha hawafanyi kosa Oktoba 25 bali wampigie kura kwa wingi.

Alisema CCM itaondoka madarakani

Aidha, aliwaomba wananchi wa jimbo la Vunjo kumruhusu mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, James Mbatia ili aweze kusaidia kuongeza nguvu katika mapambano ya kitaifa ya harakati za kuiweka Ukawa madarakani ambapo wananchi hao walimkubalia.

Ivo Aungana Na Maftah Kulaani Kitendo Cha Nyosso
24 Waitwa Kuivaa Malawi