Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amekanusha taarifa zilizosambaa kuwa aliwakingia kifua wabunge 8 wa chama hicho waliotakiwa kufukuzwa.

Awali, kulikuwa na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kukaririwa na baadhi ya vyombo rasmi vya habari kuwa Lowassa pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ndiyo waliowatetea wabunge hao nane waliokuwa kikaangoni.

“Tafadhali, sijasikia hizo taarifa [za wabunge kutaka kufukuzwa Chadema],” Lowassa alimwambia mwandishi wa EATV. “Tafadhali bwana naomba uwaulize haohao walioandika, mimi sina habari,” aliongeza.

Kikao cha Kamati Kuu kilitoa adhabu kwa wabunge hao ambao kipande cha sauti kilichorekodi mazungumzo yao kilidaiwa kuwa na maneno hasi na ya hujuma dhidi ya Meya wa Ubungo, Boniface Jacobo.

Wabunge hao walivuliwa nyadhifa zote ndani ya chama hicho kasoro ubunge na walitakiwa kuomba radhi mbele ya waandishi wa habari kuhusu kitendo hicho, masharti ambayo waliyatimiza.

Video: Daraja refu kuliko yote duniani lazinduliwa China
Leo ni leo Man Utd Vs Juventus: Sanchez nje, Ronaldo ndani

Comments

comments