Kazi kubwa iliyofanywa na Rais John Magufuli katika kipindi alichokaa madarakani hususan muelekeo wa sera yake ya kujenga Tanzania ya viwanda umewakuna wengi akiwemo aliyekuwa mpinzani wake kwenye uchaguzi mkuu, Edward Lowassa (Chadema).

Rais Magufuli ameendelea kuweka msisitizo kuwa anataka kujenga uchumi wa Tanzania kwa kufufua viwanda vilivyokufa na kujenga viwanda vipya vitakavyopeleka nchi katika uchumi wa kati.

Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa jitihada hizo za kujaribu kufufufa uchumi wa viwanda ingawa alieleza kutokubaliana na mbinu anazotumia kufikia malengo hayo mazuri.

“Rafiki zangu nawasikia na nafurahi sana wanasema wanataka kujenga nchi ya viwanda. Natamani nchi hiyo, lakini lugha hiyo sina imani nayo sana,” alisema Lowassa katika mahafali ya Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Wafuasi wa Chadema (Chaso) katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita.

“Wanasema watafufua viwanda, lakini viwanda vilivyopo vili kuwa analojia sasa hivi mambo yote ni ‘digital’. Hicho kiwanda kitafufuliwaje maana hata madukani spea zake hazipo labda zitengenezwe upya,” alisema Lowassa.

Hata hivyo, Mwanasiasa huyo mkongwe alieleza kuwa anatambua hitaji kubwa lililopo hivi sasa nchini ni ajira hasa kwa vijana ambao ni nguvu kazi kuu zaidi.

Endapo Serikali ya awamu ya Tano itafanikiwa kuvuka changamoto hizo na kufufua viwanda itaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo hilo la ajira nchini na kukuza uchumi.

Sentensi 3 za Waziri Nape kuhusu wabunge wa upinzani kususia bunge
Video: Wabunge upinzani wameendelea na huu msimamo wao