Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa juzi alikuwa katika jimbo la Monduli aliloliongoza kama Mbunge kwa miaka mingi kabla hajajieungua na kuwania nafasi ya urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambapo alisema neno kwa wananchi wake kuhusu maendeleo.

Akiongea katika sherehe za mahafari ya shule ya sekondari ya Irkisongo iliyopo Wilayani Monduli, Lowassa aliwahakikishia wananchi hao kuwa bado ataendelea kuwa pamoja nao katika shughuli za maendeleo akishirikiana na Mbunge mpya wa jimbo hilo.

“Bado nitaendelea kuyahifadhi mambo ya Monduli, ntashirikiana na mbunge si kumwangusha bali kuhakikisha maendeleo ya Monduli yanabaki palepale,” alisema Lowassa.

Alisema baadhi ya miradi ya kudumu jimboni humo ni pamoja na uwepo wa maji ya kutosha pamoja huduma ya afya kupitia hospitali kubwa itakayowafanya wananchi kutolazimika kwenda mjini kutafuta huduma hiyo.

Aidha, Mwanasiasa huyo mkongwe aliwasisitiza wananchi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanawapa watoto wao elimu kadri iwezekanavyo kwakuwa mali huisha lakini elimu ni hazina.

“Hizi fedha, nyumba na magari yataisha na kupotea,lakini elimu itabaki vichwani,” alisema.

Young Africans Kukabidhiwa Mwali Wao Mjini Mtwara
Mayanja Kuifumua Fumua Simba Na Kuiunda Upya