Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa ameonesha kushangazwa na takwimu za wapiga kura zilizotajwa na rais Jakaya Kikwete na baadaye kutolewa ufafanuzi.

Akiwahutubia wanananchi katika jimbo la Magu mkoani Mwanza, Lowassa aliitaka Tume ya Taifa Uchaguzi kuwa makini na kutenda haki kwa vyama vyote vya siasa ili wasiliingize taifa katika matatizo ya vurugu za uchaguzi.

4

“Tume ya uchaguzi ina kazi kubwa sana. Wasipoangalia watavuruga uchaguzi, na uchaguzi ukivurugwa ni mwanzo wa matatizo katika nchi. Kwa sababu, mimi sielewi… rais wa nchi anapewaje takwimu halafu baada ya masaa mawili zinakanushwa! Huyo anayempa mkuu wa nchi takwimu za namna hiyo ni nani?” Alisema Lowassa.

Mgombea huyo wa urais alionesha kutoridhishwa kwake na mwenendo wa utendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikiwa zimebaki siku 9 tu watanzania wapige kura kuwachagua rais, wabunge na madiwani.

“Tulisema Tume ya Uchaguzi ni huru, je ni huru kwa hali hii kama inatoa taarifa zinazotofautiana kwa rais?” alihoji.

3

Katika hatua nyingine, Lowassa aliwaahidi wananchi wa Magu kuwa endapo ataingia ikulu na timu ya Ukawa, atahakikisha anapambana na umasikini kwa kasi kubwa, huku akiahidi kufuta nauli kwenye vivuko vyote vya serikali nchini.

Wachezaji Wa Eritrea Watokomea Botswana
Niyonzima Hajawasili Kambini