MhadhiriMwandamizi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana amemtahadharisha mgombea urais kwa tiketi ya Chadema chini ya Ukawa kutoridhika na umati mkubwa wa watu waliomsindikiza kuchukua fomu katika makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Dk. Bana amesema kuwa umati kama huo unafanana na umati uliojitokeza kuumuunga mkono Augustine Mrema mwaka 1995 alipokuwa akigombea urais kwa tiketi ya NCCR – Mageuzi lakini alishindwa.

Alisema kuwa Lowassa anaweza kujiridhisha tu endapo umati huo utapiga kura kweli katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba na sio vinginevyo.

“Ingawa hatuwezi kupuuza umati mkubwa uliojitokeza kumsindikiza Lowassa wakati anachukua fomu katika makao makuu ya Tume Ya Uchaguzi ya Taifa, viongozi wa Ukawa na wote wanaowaunga mkono hawatakiwi kuridhika,” Alisema.

Dk. Bana ambaye ni mhadhiri mwandamizi katika kitivo cha Sayansi ya Siasa na Utawala, alisema kuwa Lowassa aliweza kuvuta umati mkubwa wa watu ambao haukuwahi kutokea kwa kuwa alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza Tanzania kuihama CCM na kuhamia nafasi ya upinzani.

FA: Kadi Nyekundu Ya Courtois Ilistahili
Pedro Ampuuza Meneja Wa FC Barcelona