Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa, leo ameingia jijini Nairobi nchini Kenya ambapo amejumuika na rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta na makamu wa Rais William Ruto katika tukio la kihistoria la kanisa la Anglikana nchini humo.

Lowassa na viongozi hao walihudhuria tukio la kusimikwa na kuwekwa wakufu Askofu Mkuu wa kanisa hilo nchini Kenya, Askofu Mkuu Jackson Ole Spit.

Lowassa Kenya

Taarifa kutoka nchini humo zimeeleza kuwa Lowassa alifanya mazungumzo na viongozi hao wakuu wa nchi baada ya kumaliza tukio hilo la kiimani, lakini mazungumzo hayo hayajawekwa wazi.

Katika tukio hilo, Rais Kenyatta alitoa wito kwa Askofu Ole Spit kufuata nyayo za mtangulizi wake na kuhakikisha kanisa linakuwa na mchango mkubwa katika vita dhidi ya ufisadi na rushwa.

“Sisi ni taifa lenye hofu ya Mungu, lakini pia tunapaswa kuwa taifa lenye mafanikio,” alisema Rais Kenyatta.

Lowassa ambaye alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho amekuwa akionekana kwenye matukio mbalimbali ya kijamii hivi karibuni huku ndoto yake ya kuzunguka nchi nzima kuwashukuru wapiga kura waliomuunga mkono ikififia baada ya Jeshi la Polisi kupiga marufuku mikutano ya kisiasa nchini.

Ukimya wa Mnyika wazua jambo, ahisiwa kumpinga Lowassa, Chadema wanena
Tanzia: Aliyekuwa Mbunge wa Kilindi, Shellukindo afariki