Viongozi waandamizi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)wamefikishwa mahakamani leo saa 2 asubuhi katika Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa dhamana yao huku wakisindikizwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati kuu CHADEMA.

Kesi hiyo ya Viongozi wa CHADEMA inatarajiwa kutajwa leo chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambaye anatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu dhamana ya washtakiwa hao.

Hata hivyo baadhi ya Viongozi wengine wa chama hicho wamefika mahakamani hapo ili kuwasindikiza viongozi wenzao wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Profesa Abdallah Safari na  baadhi ya Wabunge.

 

TRA yazindua vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo
Jeshi la Polisi lakanusha kuhusika na kifo cha mfanyabiashara