Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa ametoa ahadi juu ya kinachoendelea baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa Marudio visiwani Zanzibar.

Lowassa ambaye jana alitoa shukurani katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) Azania Front jijini Dar es Salaam, alifuatwa na wadau na waandishi wa habari ambao walikuwa na kiu ya kuupelekea umma wazo na tamko lake kuhusu kinachoendelea visiwani humo.

Mwanasiasa huyo mkongwe aliahidi kuwa atazungumzia suala hilo baada ya kuona kitakachoendelea visiwani humo na kuwataka wanahabari kutomuuliza hilo wakati huu.

“Niacheni kwanza, nitaongea. Tungoje tuone kitakachoendelea huko,” alisema.

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein tayari ameshaapishwa na ameanza kuunda serikali yake ambayo haitahusisha Chama Cha Wananchi (CUF) kwakuwa chama hicho kiliususia uchaguzi wa marudio ambao ungekiwezesha kujumuishwa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Rage Aishauri TFF Kudai Fidia Za Mchezo Dhidi Ya Chad
Dogo Janja aipiga teke shule