Waziri Mkuu mstaafu,Edward Lowassa amezuru shule ya Sekondari ya Nanja wilayani Monduli mkoani Arusha, ambayo ni miongoni mwa shule zilizoteketea kwa moto hivi karibuni.

Lowassa ambaye pia ni Mjumnbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema, aliambatana na viongozi wa Wilaya ya Monduli katika ziara hiyo na alikutana na uongozi wa shule pamoja na wanafunzi.

Mwanasiasa huyo mkongwe aliishauri Serikali kuweka mifumo ya kujikinga na majanga ya moto katika shule zake ikiwa ni pamoja na kuzijenga vizuri katika hali isiyokuwa hatarishi kwa majanga hayo.

“Napenda kuwakumbusha wakuu wa shule na viongozi kwamba ni muhimu shule zote za mabweni ziwezeshwe na zijengwe vizuri huku zikichukuliwa tahadhari zote za kujikinga na ajali kama hizi,” alisema.

Aidha, aliahidi kushirikiana na uongozi wa jimbo hilo pamoja na wadau mbalimbali wa elimu kuhakikisha wanasaidia kurudisha shule hiyo katika hali nzuri ili watoto waweze kuendelea na masomo yao kama kawaida.

Lowassa 2

Aliwapa pole wanafunzi wa shule hiyo na kuwasihi kusoma kwa bidii kwani elimu wanayoipata shule hapo ndio msingi wa maisha yao ya baadae.

Hiyo ni moja kati ya shule tano zilizoungua katika kipindi cha hivi karibuni mkoani Arusha.

Rais Magufuli amtuma Gambo Arusha
Bodi Ya Filamu Ya n'gaka Yatoa Siku Saba Kwa Pamoja Company Kuwasilisha Nyaraka Za Filamu Zake