Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa katika hafla fupi ya kumnadi mgombea wa ubunge jimbo la kinondoni Salum Mwalimu akiwa kama mgeni rasmi katika hafla hiyo na kuwaomba wananchi kumpigia kura mbunge huyo wa tiketi ya Chadema.

Kwenye hafla hiyo fupi Lowasa ameiomba Serikali kusikiliza maoni ya wananchi na kuyatendea kazi na kuyachukulia hatua stahiki.

“Ningependa kuchukua nafasi hii kuiomba serikali isikilize maoni ya wananchi. Serikali yeyote duniani huongozwa na ‘public opinion’, kwamba wanasema nini wananchi” amesema Lowassa.

Lowassa amesema kuwa haiwezekani wananchi wakawa wanasema halafu hakuna hatua yeyote inayochukuliwa na serikali, hivyo ameiomba Serikali isikilize maoni ya wananchi.

Kwa upande mwingine, Edward Lowassa amelishukuru Baraza la Maaskofu Tanzania kwa kuweza kuwaunga mkono upinzani na wapenda mabadiliko katika kutetea haki za wanyonge katika nchi.

Ndugu wa mume, mke chanzo cha ongezeko la talaka, soma zaidi kufahamu sababu nyingine
Huu ndio ukweli kuhusu ndoa ya AY

Comments

comments