Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa salamu zake za Sikuu ya Maulid kwa Waislamu wote nchini, akiwasihi kuzingatia mafundisho ya Mtume Muhammad SWA.

Amesema kuwa Waislamu nchini kama walivyo waumini wa dini nyingine, wamekuwa nguzo muhimu katika kujenga amani na upendo kutokana na mafundisho mazuri ya Mtume Muhammad SWA.

Aidha, mwanasiasa huyo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, ametumia nafasi hiyo kuwasihi Watanzania na Watawala kwa ujumla kuzingatia mafundisho ya dini kwa kuheshimiana, kuvumiliana na kupendana.

“Ni rai yangu kwa Watanzania wote wakiwemo Watawala kuwa tunaposherehekea siku hii tutimize kwa vitendo mafundisho ya Bwana Mtume ambaye ni mmoja wa mitume wa Mwenyezi Mungu kwa kuheshimiana, kuvumiliana na kupendana,” ameandika Lowassa.

Leo, Lowassa yuko mkoani Tabora akiendelea na ziara yake ya kufanya vikao vya ndani na viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi za mashina.

 

Wasichana wawili wa miaka 7 wajilipua kwa mabomu sokoni
Video: Mzee wa miaka 75 aliyeweka tangazo kutafuta mke afunguka...