Waziri Mkuu aliyejiuzuru na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa amesema kuwa licha ya changamoto nyingi anazopata akiwa upinzani atagombea tena nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 na anaamini atashinda.

Lowassa ambaye alijitokeza kugombea nafasi ya urais ndani ya CCM mwaka 2015 na jina lake kukatwa katika kura za maoni hali iliyopelekea kuhamia Chadema na kugombea nafasi hiyo ya urais akiwakilisha vyama vilivyoungana chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kushindwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli bado anatajwa kuwa ni mwenye nguvu kubwa kwa upande wa upinzani.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilimtangaza Rais Dkt. Magufuli kuwa mshindi kwa kupata kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46 huku Lowasa wa Chadema akijipatia kura 6,o72,848 sawa na asilimia 39.97 ya kura zote.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari wa National Media Group (NMG) jijini Nairobi, ambapo amesema kuwa kwa mapenzi ya Mungu atagombea tena mwaka 2020 huku akiwa na matumaini ya kushinda.

“Kwa mapenzi ya Mungu nitagombea tena mwaka 2020 na ninaamini nitashinda kwakuwa wananchi bado wananipenda na kuniamini kuwa mimi ndio nafaa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”amesema Lowassa

Hata hivyo, Lowassa yupo nchini Kenya kuhudhulia mazishi ya aliekuwa Waziri wa Usalama, Jenerali Joseph Nkaisery na kuongeza kuwa uongozi wa nchi hiyo utaamuliwa na Wakenya wenyewe katika uchaguzi.

 

 

Joe Hart Kufanyiwa Vipimo Vya Afya
50 Cent atamba kumficha Jay Z mwishoni mwa mwaka na albam mpya