Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Taifa Edward Lowassa,amewaomba marais wastaafu kuingilia kati siasa za chuki alizozisema zimeanza kujitokeza nchini.

Ameyasema hayo wakati akifunga Kampeni za Udiwani ktika kata ya Isagenhe wilayani kahama mkoani shinyanga,alipomnadi mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia Chadema Richard Luziga,amesema kuwa kadri siku zinavyokwenda baadhi ya watu wameanza kuendesha siasa za chuki huku wengine wakimtabiria kifo.

“Hizi chuki ni mbaya sana wanazielekeza kwa watu na kuzifanya ziwe mbaya zaidi,kwa mfano wapo walionitabiria kifo,lakini Mwenyezi Mungu amewatanguliza mbele ya haki kabla yangu,nasema siasa za chuki hazitusaidii kitu katika nchi hii, ni vizuri tujenge umoja na mshikamano katika nchi yetu,”amesema Lowassa.

Aidha, kwa upande wake kada wa chama hicho,Khamis Mgeja aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa shinyanga,amewataka wakazi wa kata ya Isagenhe kumchagua mgombea wa chma hicho.

Kwa upande wake Mgombea udiwani wa Chadema Richard Luziga,amewaomba wananchi wamchague  kwa kura nyingi na kwamba iwapo atashinda,mambo takayoyapa kipaumbele katika kuyashughulikia ni ujenzi wazahanati, umeme na kufikisha maji katika kata hiyo.

'Serikali imeanza kulipa madeni ya watumishi' - Majaliwa
Mbowe kitanzini tena,apewa siku 14 kulipa deni linalomkabili