Zikiwa zimebaki siku 28 wananchi wafanya uamuzi wa nani awe rais wa serikali ya awamu ya tano, mgombea urais kupitia Chadema Edward Lowassa ameonesha jinsi anavyoyasikia na kuyaona yote yanayosemwa dhidi yake na kuamua kuwaeleza wananchi namna bora zaidi ya kujibu.

Akiongea katika mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Mirirani, Simanjiro mkoani Manyara, Lowassa aliiuambia umati huo kuwa anafahamu wapo watu wanaomuandika uongo juu yake na kumtukana kwenye magazeti na sehemu nyingine, lakini akawataka wananchi hao kutowajibu kwa maneno bali wawajibu kwa vitendo kwa kumpigia kura za ndio Okotoba 25.

“Kuna watu wanaandika mambo ya uongo dhidi yangu kwenye magazeti, msiwajibu, wanatoa matusi tu, nawaomba muwajibu Oktoba 25 kwa kunipigia kura,” alisema Lowassa ambaye alieleza kuwa anatarajia kuona mafuriko ya kura.

Aidha, aliwahidi wakazi wa Mirirani kuwa akichaguliwa kuwa rais atahakikisha asilimia 50 ya pato litakalotokana na madini ya Tanzanite linawanufaisha watanzania wote.

Pamoja na mambo mengine, Lowassa aliwaahidi wananchi hao kuwa atahakikisha barabara ya KIA hadi Simanjiro inakamilika haraka, atashungulikia migogoro ya ardhi inayowakumba wakazi wa eneo hilo pamoja na kuwafikishia huduma ya maji haraka iwezekanavyo.

Magufuli Apotezea Majibu Ya Tafiti, Awaonesha Wananchi Njia Mbadala
Utafiti Mwingine Wa Septemba Wampa Lowassa Ushindi