Mheshimiwa Edward Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani ambaye ni mmoja wa watangaza nia wanaaomba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi kugombea nafasi ya kwenda kuishi Magogoni, amekamilisha safari yake ya kutafuta wadhamini.

Katika safari hiyo, Mheshimiwa Lowassa ametembelea mikoa 31 ya Tanzania Bara na Visiwani na kukusanya saini za wadhamini zaidi ya 870,000.

Akihitimisha safari hiyo mjini Morogoro, Lowassa alichukua fursa hiyo kuwashukuru wale wote waliojitokeza kumdhamini.

Comments

comments