Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi Chadema akiungwa mkono na vyama vya upinzani vilivyounda Ukawa, Edward Lowassa ameweka wazi mambo aliyozungumza na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa walipokutana hivi karibuni mjini Moshi.

Viongozi hao walikutana kanisani katika tukio la Kumuingiza kazini Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo.

Akizungumza na wazee wa Chadema jana jijini Dar es Salaam, Lowassa alisema kuwa katika mazungumzo yao, Waziri Mkuu Majaliwa alimueleza kuwa amewaruhusu kufanya mikutano nchi nzima kwa lengo la kuwashukuru Wapiga kura wao.

Lowassa alieleza kuwa baada ya kupata ruhusa hiyo kutoka kwa Waziri Mkuu, upangaji wa ratiba ya kuanza kufanya mikutano hiyo nchi nzima kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura yeye pamoja na wabunge na madiwani wa vyama vilivyokuwa vinaunda Ukawa.

Hata hivyo, mwanasiasa huyo mkongwe alisema kuwa kabla ya kuanza kwa kazi hiyo, Kamati Kuu ya Chadema imepanga kukaa na kujadili uchaguzi mkuu ili kutathmini walipokosea ili waanze kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Askofu ashusha Ombi kwa Magufuli, ataka hawa waliotumbuliwa wasamehewe
Beyonce amtumbua jipu meneja wake