Mgombea wa Chamadema anaewakilisha ngome ya Ukawa wameikejeli serikali ya CCM kwa madai kuwa imekumbuka shuka wakati tayari kumekucha.

Lowassa ameeleza hayo alipokuwa Kigoma Mjini, kufuatia kauli ya waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta kuwa serikali iko katika hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa reli ya kati, kauli iliyotolewa siku chache baada ya mgombea huyo wa Ukawa kuahidi kujenga reli hiyo pindi atakapoingia madarakani.

Akihutubia umati mkubwa wa watu mkoani humo, Lowassa aliwahidi wakazi wa mkua huo kuwa endapo ataingia madarakani atahakikisha bandari ya kigoma inakuwa bandari ya kisasa.

“Mnipe kura nikalete mabadiliko ya kweli kwa kila Mtanzania na bandani ya kigoma lazima ijengwe iwe bandari ya kisasa,” alisema na kuongeza kuwa atahakikisha unafanyika uvuvi wa kisasa katika ziwa Tanganyika.

Katika hatua nyingine, Lowassa aliwataka watu waliopewa uraia wa Tanzania kutoogopa kumpigia kura kwa kuwa amesikia taarifa kuwa wanatishiwa kuwa watanyang’anywa uraia huo endapo hawataipigia kura CCM.

“Tumesikia taarifa hizo na tumemtuma Laurent Masha (waziri wa zamani wa mambo ya ndani) afuatilie jambo hilo,” alisema.

 

Magufuli Awakamia Wahandisi
Mzee Wa Upako Anena Kuhusu Wanasisa Kuwafuata Viongozi Wa Dini