Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Lowassa amesema kuwa aliyekuwa Rais wa Cuba na mwana mapinduzi wa nchi hiyo, Fidel Castro alimhamasisha kuingia katika uongozi.

Ameyasema hayo alipotembelea ubalozi wa Cuba hapa nchini kutoa pole na kusaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Castro kilichotokea Novemba 25 mwaka huu jijini Havana nchini Cuba.

Lowassa amesema Marehemu Castro alikuwa mwana mapinduzi na ni miongoni mwa wanasiasa waliomhamasisha kuingia kwenye uongozi kutokana na alivyokuwa akiwa tetea masikini na wanyonge duniani, hali ambayo imelisababishia taifa hilo dogo kuogopwa kutokana na uimara wake.

“Castro alikuwa kiongozi imara sana,kila kiongozi makini lazima awe  kinara wa kuwatetea wanyonge na masikini popote walipo”alisema Lowassa.

Lowassa amesema kuwa Castro aliifanya Cuba pamoja na udongo wake uitikise dunia kwa kuwa kila mahali ukienda ni lazima utasikia jina la Castro.

 

Dangote aipaisha Tanzania kimataifa
Tanesco yakamilisha baraka ya Rais Magufuli kwa Bakhresa