Waziri Mkuu wa Zamani aliyejiuzuru na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa ameripoti Makao Makuu ya Jeshi la Poisi kwenye Ofisi za Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa Jinai (DCI), Robert Boaz.

Lowassa ambaye ameambatana na mkewe, Reginal na Mwanasheria wake, Peter Kibatala ameripoti Polisi hii ikiwa ni mara ya nne kuripoti hapo akituhumiwa kutoa kauli za kichochezi wakati wa futari iliyoandaliwa juni 23 na Mbunge wa Ukonga jijini Dar es salaam, Mwita Waitara.

Aidha, katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa gerezani akidai utaratibu wa kisheria ufanyike ili waachiliwe huru.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi limeweka ulinzi mkali katika eneo hilo, huku Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa akiwa ndani tayari kwa kuhojiwa na Mpelelezi wa Makosa ya Jinai.

Ni huzuni kubwa, Mama Zari Hassan afariki dunia
LIVE: Ziara ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza nchini Tanzania