Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzuru na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward lowassa anatarajiwa kuburuzwa mahakani na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi.

Hayo yamesemwa na Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Tundu Lissu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa amepata taarifa za uhakika kuwa Lowassa atafikishwa Mahakamani.

Amesema kuwa amepata taarifa za uhakika kutoka kwa chanzo cha kuaminika ndani ya Jeshi la Polisi kwamba taratibu za kumfikisha mahakamani zinafanyika na uko katika hatua za mwisho.

“Nimepata taarifa tena kwa polisi mwenye cheo kikubwa tu ndani ya Jeshi hilo kwamba utaratibu unafanyika wa kumfikisha Lowassa mahakani na watamshtaki kwa kosa la uchochezi,”amesema Lissu

Hata hivyo, Rais Dkt. John Magufuli aliwaonya wanasiasa na kuvitaka vyombo vya dola kuwakamata wale wote wanaowatetea masheikh wa Uamsho ili wasaidie polisi katika uchunguzi bila kujali anatembea taratibu, haraka wala cheo.

 

Kendrick Lamar amzawadia shabiki mlemavu toleo jipya la gari maalum
Man United yaendeleza ubabe Marekani

Comments

comments