Mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa leo ametakiwa kuripoti katika ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya jinai (DCI), Robert Boaz.

Lowassa, ambaye alikuwa mgombea urais wa Chadema, kupitia vyombo vya habari alithibitisha kuwa ameambiwa afike katika ofisi hiyo leo saa nne asubuhi.

Lowassa amesema hajui anachoitiwa, lakini anahisi ni kutokana na ushauri alioutoa kwa Rais Magufuli kumtaka  awaachie huru viongozi wa jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya kiislamu Zanzibar (Jumiki), waliokamatwa tangu mwaka 2012.

Taarifa hiyo ilisema Lowassa alitoa ombi hilo jijini Dar es salaam alipozungumza katika futari iliyoandaliwa  na Mbunge wa Ukonga (Chadema) Mwita Waitara.

”Ni kweli nimetakiwa niripoti kesho (leo) saa nne asubuhi katika ofisi ya DCI. Sijui wananiita nini, lakini nahisi ni kuhusu nilichosema juu ya masheikh wa Uamsho,” amesema Lowassa.

”Nilisema hivyo kwa sababu kuna Sheikh wakati wa kunikaribisha alisema japo tunasherekea Eid el Fitr bado kuna masheik wenzetu wanateseka. Nilisema hivyo kwa sababu nilishaahidi kwenye kampeni zangu kwamba tukishinda tutawatoa hao masheikh,” amesema Lowassa.

Robert Boaz, ambaye ni DCI amesema swala hilo aulizwe msemaji wa jeshi la Polisi, Advera Bulimba, ambaye pia kwa upande wake alisema hilo swala mzungumzaji mkuu awe Lowassa mwenyewe.

 

Rais wa Brazil kikaangoni, aburuzwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi
Video: Mchujo mkali mauaji Kibiti, Lowassa aitwa Polisi kuhojiwa