Wakati mbio za uchaguzi mkuu zikiendelea huku mengi yakiibuliwa kila kona kama mbinu za ushindi, mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa ameibuka na mpango mpya endapo atapewa ridhaa ya kuingia madarakani.

Lowassa ambaye anagombea urais chini ya mwanvuli wa Ukawa ameahidi kuwa endapo ataingia ikulu atalifanyia uchunguzi upya sakata la mauaji uharibifu wa mali za wananchi uliyotokana na operesheni tokomeza ujangili.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Mpanda, Lowassa alisema kuwa ataunda tume mpya itakayochunguza sakata hilo kwakuwa wapo wananchi wanaolalamika hadi wakati huu kuwa licha ya kuathirika vibaya na operesheni hiyo bila hatia, hawakulipwa fidia.

“Wananchi wengi wamekuwa wakija kuniona kuhusu operesheni tokomeza Ujangili na kunieleza wazi kuwa licha ya madhara yaliyojitokeza katika operesheni hiyo hawakulipwa, pia walipoteza haki zao, ndugu na mifugo,” alisema.

Mwaka 2013, waziri wa maliasili na utalii, Lazaro Nyalando ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali katika kupambana na ujangili nchini. Hata hivyo, bunge liliamua kusitishwa kwa operesheni hiyo na kuunda tume maalum iliyokuwa chini ya mbunge wa Kahama, James Lembeli ambayo ilibaini ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Mgombea huyo pia ameahidi kuunda tume nyingine mbili zitakazochunguza na kushughulikia migogoro ya ardhi  kati ya wananchi na wawekezaji pamoja na migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.

 

 

 

 

 

Profesa Lipumba: Mimi, Dk Slaa Ndio Wapinzani
AVB Kuishuhudia Zenit Akiwa Jukwaani