Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa, amesema kuimarika kwa umoja na mshikamano miongoni mwa vyama vya upinzani nchini kunawatia kiwewe Chama cha Mapinduzi (CCM), wanaoongoza serikali na kufanya waanzishe mbinu chafu za kisiasa.

Aidha, Lowassa amesema kuimarika kwa mshikamano huo chini ya mwamvuli unaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ni hatua kubwa katika safari ya kuiondoa CCM madarakani na kuingia Ikulu ili waweze kuongoza dola.

“Wameanza mbinu chafu za kutuondoa kwenye umoja wetu kwa kuwalisha viongozi wetu maneno, kuna gazeti moja limenilisha maneno likidai kuwa eti nimeitabiria CCM ushindi katika uchaguzi mdogo wa Udiwani kule Arumeru, haya ni mambo ya ajabu kabisa, linaishi kwa kodi zetu wananchi leo linatumika kuvunja Demokrasia,hili ni jambo la kusikitisha,”amesema Lowassa.

Lowassa amesema lengo la ziara hiyo wanayofanya ni kuimarisha chama na kuimarisha mshikamano miongoni mwa wapinzani wa CCM ambao wanapata kiwewe na kusisitiza kuwa hata iweje mabadiliko ni lazima.

Hata hiyo Lowassa alipata nafasi ya kusalimiana na wananchi mbalimbali akiwa njiani kuelekea mkoani kagera kwaajili ya ziara ya kuimarisha chama.

AFCON 2019: Hatma Ya Tanzania Mikononi Mwa Uganda, Cape Verde, Lesotho
Video: Tuhuma za rushwa ajira 600 Dangote, JPM ajibu mapigo...